Saturday, 14 May 2016

FAHAMU MBINU BORA ZA KILIMO CHA MITI 2016

Wakati tunaelekea kwenye kipindi cha kuanza kupanda na kuotesha miti mipya ya msimu wa 2014- 15 ambao huanza rasimi mwezi wa 12 wa kila mwaka, watu wengi sana walitutumia email na kutupigia simu, kulizia taratibu za kupata maeneo ya kupata mashamba, na wale wenye mashamba walitupgia kuulizia namna ya kupata miche ama kununua mashamba yenye miti zaidi ya yale waliyonayo kwa sasa. Makala hii fupi inafafanua kwa undani zaidi, hii ni kwa faida ya watu wengine. 


Unaweza kununua mashamba yenye miti tayari kwa mchanganuo ufuatao: 


Miti pamoja na ardhi: Miti ya mwaka mmoja = 600,000 Miti ya miaka 2 = 700,000 hadi 800,000 (bei zinatofautiana kutokana
na ‘location’ yalipo mashamba husika). 


Mashamba ambayo hayana kitu (yasiyo na miti) huuzwa kwa shilingi laki 200,000/ kwa ekari. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni shilingi laki mbili kwa ekari moja.


Hata hivyo unaweza kupata mashamba haya yenye miti kwa bei za chini zaidi ya hizo kutegemea na wenyeji unaokutana nao pamoja na maeneo husika na idadi ya ekari unazonunua.


Ukinunua shamba tupu itakugharimu wastani wa shilingi laki tatu hadi nne katika kuandaa shamba hadi kupanda. Kwa ushauri wetu tunakushauri kama ukiweza ni vema kutafuta mashamba yenye miti tayari, ununue. HII itakusaidia kuepusha usumbufu wa kuandaa na kupanda hadi ishike ardhini. Ukishanunua shamba iwe ni kutoka kwetu ama kwa wenyeji, kunakuwa na ‘documents’ ambazo zinatolewa na serikali ya kijiji husika kwa idhini ya kamati ya ardhi ya kijiji.


Kwa upande wetu (ikitokea unanunua kutoka plots za kampuni) mara zote management fee tunaijumlisha katika bei ya manunuzi. Kitu ambacho utaendelea kufanya ni kugharimia uhudumiaji wa shamba ambao una shughuli kubwa mbili; 1) Kuproon-wastani wa shilingi laki moja kwa ekari na inafanyika mara mbili hadi tatu kuanzia kupanda hadi kuvuna. 2) Kutengeneza njia kuzunguka shamba na inafanyika kila mwaka na ni wastani wa shilingi elfu sitini kwa ekari moja.


Miti ipo ya aina tofauti. Kwa hapa Iringa kuna miti ya aina mbili inayostawi; ya (nguzo na mbao) iitwayo milingoti naya (karatasi na mbao) iitwayo Pines. Hii ya milingoti inachukua muda mfupi zaidi kukua (wastani wa miaka mitano hadi saba ikiwa ni kwa matumizi ya nguzo na mirunda hutumia miaka miwili hadi mitatu) na pines ambayo ni maalumu kwa ajili ya mbao na kutengenezea karatasi inachukua miaka 7 hadi kumi mpaka kuvunwa.


Ekari moja inachukua miche 500 mpaka 600 na ‘survival rate’ ya aina zote mbili nilizokutajia ipo asilimia 80%. 


Uvunaji upo wa aina mbili. Unaweza kuamua kuuza miti kama miti (yaani magogo) ambapo kwa miti hii ya nguzo kwa mti mmoja uliokomaa vizuri unauzwa kuanzia 20,000 na kuendelea. Kwa upande wa miti ya mbao na karatasi mti uliokomaa vizuri unauzwa kuanzia 20,000 na kuendelea (ingawa hii pia inaamuliwa na ‘location’ ya shamba. Shamba linapokuwa mahali kusikofikika bei ni ndogo zaidi). Namna ya pili ya uvunaji ni kuvuna mwenyewe kwa maana ya ama kupasua mbao au kutengeneza nguzo za umeme za kuuza. Katika hii ‘option’ ya pili ya uvunaji inakulazimu uwe katika biashara kamili ya mbao kwa sababu utahitaji mashine, leseni, vibali na taratibu nyingine. 


Hadi sasa tunavyoongea, hali ya soko la mbao na nguzo/mirunda liko juu sana na demand ni kubwa kuliko supply. Nadhani unatambua kuwa mahitaji ya bidhaa za miti yameongezeka kwa kasi sana miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika na wataalamu wakiwemo SUA wanatueleza kuwa soko la bidhaa za misitu (mbao, nguzo n.k) litaendelea kupanda bila kushuka kwa miaka 25 ijayo kuanzia mwaka 2010. Kama wawekezaji tunakuwa positive katika hilo ijapokuwa hatuachi kuweka tahadhari ya risks (ikiwemo market changes) kama ambavyo ni kawaida kwa biashara yeyote duniani


Ninaamini nimekupa ufafanuzi mzuri na mahali popote ambapo utakuwa hujapaelewa ama unahitaji ufafanuzi zaidi usisite kuwasiliana nami. Ni furaha yangu ukisaidika na kufanikiwa.


Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara katika makala zangu; ni kwamba muda wa kulalamika lalamika umekwisha. Mazoea na utamaduni wa watanzania wengi kudhani kwamba tunaonewa wakati wote haujatusaidia mpaka hapa kwa jinsi hii hakuna sababu ya kuendelea nao. 


Mtindo wa kuishi maisha ya kutaka kuhurumiwa yanatupotezea muda wenye thamani. Tumekuwa tukilalamika kuwa wageni (wanaokuja kwa jina la wawekezaji) wanatupora ardhi; lakini tusichokitafakari ni hiki, “Mimi kama mtanzania kwa nafsi yangu na kwa uwezo wangu nimefanya nini cha maana katika ardhi ninayoweza kuipata hapa nchini ama ninayomiliki?”.

KILIMO CHA MITI YA MBAO,NGUZO NA MATUNDA IRINGA NA NJOMBE


Kilimo cha miti kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mikoa ya Njombe na Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa.



Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi. Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa (carbon dioxide). Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.



Hii ni sawa na kutegeneza hela ukiwa umelala. Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo, karatasi ama mbao.Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.

Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi kitabu hiki ni kukupa taarifa hizi za utajirisho. Miti ya mbao inatumia wastani wa miaka sita hadi 8, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake.



Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000, inategemea na ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na nane (18,000,000). 



Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni thelathini na mbili (32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji (demand) wa mbao katika soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi. 

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi elfu Themanini na laki moja na 20 elfu (120,000) kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki moja na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki nne tu! Kutegemea na umri wa miti unayotaka. 

Mtu unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo Asasi ya PDPR imekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitatu na miaka minne.



Uponunua mashamba haya kutoka kwetu, PDPR inaendelea na upandaji wa mashamba mapya kupitia fedha hizo. Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako.



Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning).



Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima. Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa shilingi laki tano. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo. 

Hata hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha. 


Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasi ya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili au mitatu.



Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono. 

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini Njombe au Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda huko, Je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?

Ili kutimiza ndoto yangu hiyo tumeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa. Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nasi kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya uzalishaji katika ardhi yetu.



Inawezekana! Kwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako itimie.